February 22, 2016

                         

Baada ya kuvuja kwa sauti ya Dogo Janja akilalamika (kwa demu) kuhusu
uongozi wake wa Tip Top connection kumbania, Madee ametoa uamuzi
walioamua kuuchukua.

Madee alianza kwa kusema kuwa hakuwa na taarifa yoyote juu ya malalamiko
yoyote ya Dogo Janja kubaniwa mpaka alipokutana nayo kwenye audio hiyo
iliyosambaa mitandaoni, na kuongeza kuwa siku moja kabla ya audio hiyo
kuvuja alikuwa na Dogo Janja wakimalizia video ya wimbo wake mpya na
hakujua kama kuna tatizo lolote.

“Mimi nabaki kwenye maamuzi ambayo tumeshaongea na Tale, kwamba
hatuwezi kutoa maamuzi ambayo wao wanadhania yatakuwa ni ya kumkandamiza
moja kwa moja Dogo Janja, kwa sababu sawa, mwanaume kama mwanaume
unapoamua kutongoza unatumia mbinu zako nyingine nyingi tu, yeye ndio
ile mbinu ambayo aliona anaweza.”/ alisema Madee.

“Lakini kama kazi zake sisi tumezifanya na tumeshafanya kila kitu video
tayari kwahiyo sidhani kama kweli yale maneno yametoka moja kwa moja
kwenye moyo wake kina Madee wananibania wakati tayari kazi zake
zimeshafanywa na ratiba yake imeshafanywa, nachoamini mimi ni kwamba
alikuwa anataka kumuwin tu Yule mwanamke, lakini kikubwa ambacho
amehaaribui ni matusi pamoja na kutoa siri ambazo yeye anaona ni sawa
kuzisema.” Alieleza Madee.

Licha ya Janjaro kufanya hayo, Madee amesema kuwa hawatasitisha kutoa
kazi zake ambazo tayari zilikuwa kwenye ratiba ya kutoka.

“ratiba lazima ziendelee kwasababu tayari tumeshapata hasara tumeshatoa
hela za kufanya audio , video ratiba itaendelea lakini lazima Dogo Janja
atakuwa chini ya adhabu.” alisema Mdee

Chanzo: Bongo 5.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE