February 28, 2016

  
Kufuatia kauli ya chama cha mapinduzi CCM ya kulitaka jeshi la Polisi  visiwani Zanzibar kumkamata Katibu mkuu wa CUF Maali Seif Sharif Hamad kwa madai ya kujitangazia ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika October 25 2015 nchini kote, Chama cha wananchi CUF kupitia kwa Ismail Jussa kimetoa tamko hili

"Maalim Seif Sharif Hamad amesema haogopi kukamatwa kama walivyoagiza CCM katika taarifa yao ya jana na amewataka Polisi wamsubiri Uwanja wa Ndege wa Zanzibar tarehe 4 Machi, 2016 siku anayorejea Inshallah ili watekeleze agizo hilo la CCM.
Tunazo pia taarifa kwamba viongozi wa CCM wametaka Polisi iwakamate Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, Ismail Jussa, Mansoor Yussuf Himid na Eddy Riyami.
Na sisi pia tunawakaribisha Polisi watekeleze maagizo hayo na watukamate.
Viongozi wa CUF kukamatwa, kuwekwa ndani, kubambikiziwa kesi na kupandishwa Mahkamani limekuwa ni jambo la kawaida tokea mwaka 1992 pale mfumo wa vyama vingi vya siasa ulipoanzishwa tena hapa Zanzibar
HATUTISHIKI WALA HATURUDI NYUMA! NA TUNAWAAMBIA TENA CCM HAINA MANUSURA"!

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE