February 08, 2016

                             
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein ameitaka jamii nchini kupambana na ukatili na udhalilishaji wa watoto kwa vitendo na sio kukemea pekee.

Dr. Shein ametoa changamoto hiyo huko mkoa wa kaskazini Unguja wakati akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi na kuizindua rasmi kazi ya ujenzi wa jengo la mahakama maalum ya kusimamia kesi zinazohusu watoto ambapo amesema vita hivyo ni vikubwa na jamii lazima iungane pamoja huku akionekana kushangazwa na watu wenye tabia hizo za kubaka na kudhalillsha watoto.

 

Mapema jaji mkuu wa Zanzibar Mhe Othman Makungu amesema kuwepo kwa jengo hilo kutapunguza misongamano wa kesi katika mahakama kuu huku akisema jengo hilo litakuwa maalum na watoto watakuwa huru bila ya uoga huku mrajis wa mahakama kuu Mhe George Kazi amesema jengo hilo linatarajiwa kumalizika mapema mwezi ujao na shilingi miloni 100 zinatarajiwa kutumika na mipango iko mbiono kwa pemba kuwa na mahakama kama hiyo.

 

Kesi za udhalilishaji na ubakaji wa watoto ni moja ya tatizo sugu kiswani Zanzibar huku tathmni zikionyesha kesi za jinai zinazohusu watoto zimefunguliwa kati ya hizo 54 za makosa ya jinsia na udhalilishaji kijinsia watoto ingawa pamekuwa na mafanikio ya kuwepo kwa wananchi kuripoti matukio 1049.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE