February 08, 2016

                    

Rais Magufuli ameyaeleza hayo katika hotuba yake kwa mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania iliyosomwa kwa niaba yake na waziri wa mambo ya nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda na kimataifa Balozi Augustine Mahiga leo ikulu jijini Dar es salaam.

Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli amewaeleza mabalozi hao kuwa licha ya Tanzania kuwa nchi moja, Zanzibar ina mfumo wake wa siasa, ina serikali yake, Katiba yake na pia tume yake ya uchaguzi inayojitegemea.

Amesema tume hiyo ilifuta uchaguzi kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kisiwani Pemba, na kwamba tayari tarehe mpya ya uchaguzi wa marudio imekwisha tangazwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

Amesema mazungumzo ya kutatua mgogoro huo yalifanyika bila mafanikio ambapo chama kikuu cha upinzani (CUF) kimeendelea kupinga uchaguzi wa marudio huku vyama vingine kikiwemo chama tawala vikionesha uhitaji wa uchaguzi huo wa marudio.

Amesema kwa hali ilivyo, busara inahitajika ili kunusuru suala hilo, na kwamba kususia uchaguzi siyo suluhu bali kutumia nafasi iliyopo sasa kujadili namna ya kuufanya uchaguzi wa marudio kuwa huru na wa haki.

“Tunakiasa chama cha CUF kama ambavyo watanzania wengi wangependa kuona, kuthibitisha madai ya ushindi wao katika sanduku la kura, hakuna jinsi nyingine ya kutatua suala hili zaidi ya kukubali kufanya uchaguzi wa marudio” imesema sehemu ya hotuba hiyo.

Magufuli amewahakikishia mabalozi hao kuwa nchi ni salama na hali ya amani na utulivu ni ya kuridhisha katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi wa marudio.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE