February 09, 2016

                        
Polisi wanasema watu wawili wamefariki

Watu wanane wamethibitishwa kufariki na wengine wengi kujeruhiwa baada ya treni mbili za kubeba abiria kugongana katika jimbo la Bavaria nchini Ujerumani.

Ajali hiyo imetokea katika mji wa Bad Aibling, takriban kilomita 60 kusini mashariki mwa mji wa Munich.

Polisi wa Bavaria wameandika kwenye Twitter kwamba watu wanane wamefariki, watu zaidi ya 50 wakaumia vibaya na takriban watu 100 wana majeraha madogo.

MOJA KWA MOJA: Ajali ya treni Ujerumani

Moja ya treni hizo ilitka kwenye reli baada ya ajali hiyo na mabehewa yake yakabingiria, vyombo vya habari nchini Ujerumani vinasema.

                        
Maafisa wengi wa huduma za dharura wametumwa eneo hilo

Inaaminika magarimoshi hayo yaligongana ana kwa ana.

Maafisa wa kutoa huduma za dharura wamefika eneo la ajalii na helikopta zinatumiwa katika uokoaji.

Barabara zilizo karibu na eneo hilo zimefungwa, sawa na njia ya reli kati ya miji ya Holzkirchen na Rosenheim.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE