March 29, 2016

 
 
Tajiri mmoja alitaka kufanya sherehe na kuwaalika marafiki zake. Akaandaa kila aina ya chakula lakini hakuweza kupata Samaki, hivyo akatoa zawadi kwa yoyote atakayemletea Samaki ili sherehe yake ikamilike.

Baada ya muda kidogo Mvuvi mmoja akaleta Samaki mkubwa sana lakini alipofika getini kwa yule tajiri Mlinzi wa pale getini hakumruhusu aingie ndani kama hatomuahidi kumpa nusu ya faida atayopata kwa Tajiri.

Mvuvi akakubali. Tajiri akafurahi sana na akataka kumpa hela nyingi lakini mvuvi akakataa kuchukua pesa hizo ila yeye akataka achapwe viboko mia moja. Kila mtu alishangazwa na uamuzi huo.

Mwisho wa mashauriano. Tajiri aliamuru mfanyakazi wake amchape viboko mia moja yule Mvuvi. Mvuvi alipotimiza viboko hamsini akamwambia mfanyakazi wa Tajiri aishie hapo kwa kuwa alishirikiana na mwenzake ambaye naye ingefaa apate nusu ya malipo hayo.

Alikuwa ni yule Mlinzi getini. Tajiri akaelewa mchezo mzima. Akaamuru mlinzi achapwe viboko hamsini vilivyobaki na akampa Mvuvi zawadi kubwa ya fedha.
Imeandikwa na Mrisho Mpoto

Umejifunza Nini? #INUKAENDELEA

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE