Amavubi Stars ya Rwanda imeweka bayana ari yake ya kufuzu kwa dimba la mataifa ya Afrika itakayoandaliwa mwakani huko Gabon.
Rwanda iliinyeshea Mauritius mabao 5-0 kwa nunge katika mechi ya marudio iliyochezewa mjini Kigali leo jioni.Ernest Sugira alifunga mabao mawili ya haraka na kuwaweka wenyeji hao kifua mbele katika mechi hiyo ya kundi H.
Vijana hao wa kocha Johnny McKinstry hawakutosheka na hayo ,Dominique Nshuti alihakikisha timu yake imekwenda mapumzikoni ikiongoza kwa mabao 3-0.
Baada ya mapumziko Fitina Omborenga na Jean-Baptiste Mugiraneza walifuta machungu ya kichapo cha 1-0 walichopata katika mkondo wa kwanza siku tatu tu zilizopita.
Katika matokeo mengine, Ethiopia ilitoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Desert Foxes ya Algeria mjini addis Ababa.
Algeria ambao wanaongoza kundi lao walilazimika kufanya kazi ya ziada baada ya wenyeji wao kuongoza mara mbili.
Algeria waliichapa Ethiopia, 7-1 mjini Blida timu hizo zilipokutana Ijumaa iliyopita katika mkondo wa kwanza.
Licha ya matokeo hayo Algeria wanaongoza kundi J na alama 10 5 zaidi ya Ethiopia.
Hata hivyo timu mbili zilizomaliza na alama nyingi katika nafasi ya pili pia zitajiunga na mwenyeji katika kindumbwendumbwe hicho.
Huu hapa mukhtasari wa matokeo ya mechi zilizochezwa leo.
#AFCON2017Rwanda 5-0 Mauritius
Namibia 1- 3 Burundi
Malawi 1-2 Guinea
Togo 0-0 Tunisia
Angola 0-1 DR Congo
Liberia 2-0 Djibouti
Uganda 0-0 Burkina Faso
Ethiopia 3-3 Algeria
Niger 1-2 Senegal
Namibia 1-0 Burundi
Togo 0-0 Tunisia
Lesotho 1-0 Seychelles.
Namibia 1- 3 Burundi
Malawi 1-2 Guinea
Togo 0-0 Tunisia
Angola 0-1 DR Congo
Liberia 2-0 Djibouti
Uganda 0-0 Burkina Faso
Ethiopia 3-3 Algeria
Niger 1-2 Senegal
Namibia 1-0 Burundi
Togo 0-0 Tunisia
Lesotho 1-0 Seychelles.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment