Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza majina 22 ya wajumbe wa viti maalumu wa Baraza la Wawakilishi, wote kutoka CCM.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jecha Salim
Jecha, wajumbe hao ni Salama Aboud Talib, Shadya Mohamed Suleiman,
Bihindi Hamad Khamis, Salma Mussa Bilal, Mwanaidi Kassim Mussa, Panya
Ali Abdalla, Mgeni Hassan Juma na Zaina Abdalla Salum.
Wengine
ni Salha Mohammed Mwinyijuma, Zulfa Mmaka Omar, Lulu Msham Abdalla, Wanu
Hafidh Ameir, Saada Ramadhani Mwenda, Tatu Mohamed Ussi na Amina Idd
Mabrouk.
Jecha aliwatangaza wawakilishi wengine wa viti maalumu
kuwa ni Choum Kombo Khamis, Mtumwa Suleiman Makame, Mwantatu Mbaraka
Khamis, Riziki Pembe Juma, Viwe Khamis Abdalla, Hamida Abdalla Issa na
Hidaya Ali Makame.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment