Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania M: dr. John Pombe Magufuli amesema kama kuna mtu ataona mshahara ni mdogo basi mapema na aanze kutafuta kazi sehemu nyingine.
"Hatuwezi kuendelea kulipana mishahara minono kiasi hicho katikati ya wananchi wanaoishi katika lindi la UMASIKINI"
Mhe. rais aliyasema haya alipokuwa Chato, aliposisitiza kuwakata mishahara wakuu wa mashirika ya Umma wanaojilipa Tsh. 40m kwa mwezi. Amesema atashusha mishahara hiyo kwa asilimia 63 na kufikia Tsh. 15m.
Pia Rais Magufuli ameahidi kushusha kodi ya mshahara hadi kufikia tarakimu 1, yaani kwenye bajeti ijayo ya mwaka mpya wa fedha kila mfanyakazi atalipa kodi isiyozidi asilimia tisa (9%)
0 MAONI YAKO:
Post a Comment