Kiungo
mchezeshaji wa zamani wa Al Masry ya Misri na Esprance ya Tunisia na
kocha wa Simba kwa sasa, Mganda, Jackson Mayanja ‘Mia Mia’, amesema
kitakuwa ni kichekesho cha mwaka kama Yanga itafungwa na Al Ahly ya sasa
ambayo anaiona ‘vibonde’.
Licha
ya uhasimu mkubwa kati ya timu yake na Yanga, lakini hilo si kigezo kwa
Mayanja ambaye amesema Yanga ina bahati kubwa kwani Al Ahly ya sasa si
ile anayoifahamu.
Imebadilika
sana na ubora wao uko chini na kuongeza kuwa Yanga wana nafasi ya
kuwondoa lakini kama kweli watajiandaa vema kutokana na asili ya soka la
Kiarabu.
Yanga
itaikaribisha Al Ahly Aprili 9, mwaka huu kwenye Ligi ya Mabingwa
Afrika, hata hivyo, takwimu zinaonyesha mara ya mwisho Waarabu hao
walikubali kichapo kwenye Uwanja wa Taifa kabla ya kulipa kisasi huko
kwao Cairo kisha kupenya kwa mikwaju ya penalti.
“Kitakuwa
kichekesho kama Yanga itakubali kupoteza kwa Al Ahly hii ambayo
nimeishuhudia mara kadhaa. Si ile Al Ahly ya Kiarabu niliyoijua, ile
ilikuwa Al Ahly kweli, imejaza wachezaji mastaa ambao usingependa
kukutana nao.
“Lakini
nadhani machafuko ya kisiasa yamewaathiri sana, wanajipanga upya na
bado hata ukiangalia mechi zao za hivi karibuni, utaona kabisa haina
ubora ule wa asili ya soka la Kiarabu,” alisema Mganda huyo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment