Rais John Magufuli amemtembelea na kumjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam, ambako anapata mapumziko baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Hindu Mandal alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Pamoja na kumpa mkono wa pole, Rais Magufuli amemuombea Maalim Seif
Shariff Hamad kupona haraka ili aweze kuendelea na shughuli zake kama
kawaida.
Kwa upande wake Maalim Seif Shariff Hamad amemshukuru Rais Magufuli
kwa ukarimu na upendo aliouonesha kwa kumtembelea hotelini hapo, na
amewahakikishia watanzania kuwa hali yake sasa inakwenda vizuri na
inazidi kuimarika
Maalim Seif alilazwa kwa siku kadhaa hospitali ya Hindu Mandal baada
ya kuzidiwa wakati akitokea Zanzibar kuja Dar es salaam siku chache
tokea kuwasili nchini akitokea nchini INDIA kwa matibabu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment