March 13, 2016

Screen Shot 2016-03-13 at 6.18.46 PM 

Watu watatu wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa vibaya katika eneo la sakina jijini Arusha, baada ya basi linalo milikiwa na kampuni ya Saibaba lililokuwa katika majaribio kugongana uso kwa uso na lori ambalo lilikuwa likitokea eneo la Oldonyosambu wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Basi hilo lenye usajili namba T 720 ADE lililigonga na lori hilo lenye usajili namba T742 CRS ambapo kwa mujibu wa Mashuhuda wa ajari  hiyo ,wanadai  ajali hiyo ilitokea majira ya saa tisa alfajiri wakati  basi la Saibaba lilipokuwa likifanyiwa majaribio na fundi aliyejulikana kwa jina la Athuman sadiki naghafla lilizimika taa zote za mbele na kupoteza mwelekeo na ndipo lilipo ligonga lori hilo lillilokuwa limebeba shehena ya karoti.
Hata hivyo inadaiwa kuwa marehemu na majeruhi wote  walikuwa abiria wa lori.
Channel ten inafanya jitihada za kufika katika hospital ya  mkoa wa Arusha mount meru ambapo uongozi wa haspitali hiyo unashindwa kutoa ushirikiano wa aina yoyote licha ya majeruhi na miili ya marehemu kuripotiwa kufikishwa katika hospital hiyo huku kamanda wa jeshi lapolisi mkoa wa arusha Liberatus Sabasi akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na tayari dereva wa basi anashikiliwa na jeshi hilo.
Kwa mujibu wa kamanda Sabasi majina ya marehemu hao ni Nouvel Joseph ambaye ndiye  alikuwa  dereva wa lori hilo wengine ni ,james kaaya na paschal peter  wote wakiwa abiria katika lori hilo.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE