Vilabu vitatu vikuu katika ligi kuu
ya Uingereza EPL vimekanusha madai kuwa wachezaji wao wanatumia madawa
yaliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu mwilini.
Vilabu hivyo vimekanusha madai hayo yaliyochapishwa na jarida la Sunday Times kuwa ya ''uongo''Jarida hilo limechapisha ripoti ya ufichuzi inayodai kuwa daktari mmoja mwenye zahanati ya kibinafsi mjini London Mark Bonar amekiri kuwapa madawa yaliyopigwa marufuku wachezaji 150 katika kipindi cha miaka 6 iliyopita.
Uchunguzi pia umebaini kuwa dkt Bonar amekuwa akiwapa wachezaji nyota dawa aina ya EPO, Steroids na hata homoni zinazokua kwa haraka.
ARSENALKlabu ya Arsenal imesikitishwa na ''madai hayo ambayo hayana msingi wowote''
CHELSEAHuko Stamford Bridge habari hizo zimepokewa kwa ''mshangao mkubwa'' huku mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya EPL wakisema ni madai tikutumia huduma za daktari Bonar anayetajwa,
u ambayo hayana msingi wowote''
''Hatujawah
'Kwa ufupi hatuna kumbukumbu zozote zinazothibitisha kuwa mchezaji wetu yeyote anatibiwa na dkt Bonar wala anayehudumiwa naye'' taarifa ilisema.LEICESTER
Vinara wa ligi kuu hiyo ya EPL Leicester nao hawakusazwa,
wamepinga kuwahi kutumia madawa hayo ya kututumua misuli wala kusajili huduma za daktari huyo anayetuhumiwa.
''Tumepigwa na butwaa kuwa jariba lenye hadhi ya Sunday Times linaweza kuchapisha tuhuma kama hizi dhidi ya wachezaji wa ligi kuu ya Uingereza ikiwemo klabu yetu ya Leicester City bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha''
''Ikiwa wenyewe wamekiri kuwa hawana ushahidi wa kutosha kwanini basi wachapishe madai haya'' ?
WADA
Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kupambana na kuenea kwa matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku nchini Uingereza UKAD bwana Nicole Sapstead amelezea kufadhaishwa na ripoti hizo akisema kuwa wataanzisha uchunguzi huru kuhusu madai haya.
''Tumeshangazwa na kushtushwa mno na ripoti hii'' bila shaka tutaanzisha uchunguzi dhidi ya madai haya.
Naye kiongozi wa shirika linalopigana na ueneaji wa matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku duniani WADA bw Craig Reedie ameiambia BBC Radio 5 kuwa ni habari za ''kuogofya sana''
''Bila shaka tutafanya uchunguzi,ila tutasubiri kwanza ripoti ya shirika husika la Uingereza UKAD kabla ya kufungua upelelezi wetu wa kina, sharti tupate ufumbuzi wa swala hili''
''Ninaamini kuwa kama UKAD wangekuwa na ushahidi wa kutosha bila shaka wangalichukua hatua madhubuti'' alisema bw Craig Reedie
Gazeti la Sunday Times limechapisha ripoti hiyo ya ufichuzi leo ikidai kuwa sio tu wasakataji dimba waliopewa madawa hayo ya kusisismua misuli bali hata waendesha Baiskeli, wachezaji Kriketi na hata wachezaji wa Tenisi maarufu wamekuwa wakipokea matibabu kutoka kwa daktari mmoja ambaye anamiliki zahanati ya kibinafsi mjini London dkt Bonar.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment