Hatimaye staa wa Bongo Muvi, Aunt Ezekiel Grayson amefanya
kila liwezekanalo na kujinasua mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dk.John Pombe Magufuli ‘JPM’ kwa kukomboa gari lake aina ya
Audi lililokuwa limeshikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa
kushindwa kulipa kodi.
Gari
la Aunt Ezekiel aina ya Audi.Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa
mbwembwe kibao wikiendi iliyopita, Aunt alimshukuru Mungu kwa kumnasua
kwenye soo hilo kwani alikuwa akiishi kwenye lindi la mawazo kwa zaidi
ya wiki tatu tangu gari hilo likamatwe.
“Namshukuru
Mungu kwa kuniwezesha kutoa shilingi milioni 15 na hatimaye nimekomboa
gari langu ambalo lilikuwa kwenye hatihati ya kupigwa mnada na TRA,”
alisema Aunt.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment