Msanii
wa muziki na mwigizaji, Baby Joseph Madaha, ‘Baby Madaha’ baada ya
ukimya wa muda mrefu amejipanga kuachia wimbo wake mpya ‘Corazon’.
Madaha
amesema kwa sasa anamalizia video ya wimbo huo ambao picha zake
zinapigwa huko Dubai na unatarajiwa kukamilika mwezi ujao.
“Nipo
kwenye harakati za mwisho za kukamilisha video ya wimbo wangu mpya wa
‘Corazon’ unaomaanisha moyo wangu ambao nimeufanyia Dubai na ninaomba
mashabiki wangu waendelee kuniombea ukamilike kama nilivyopanga,” Baby
Madaha aliliambia gazeti la Mtanzania.
Madaha alisema wimbo;huo ameurekodia katika studio za C9 Record chini ya prodyuza, C9 Kanjenje.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment