Kitenge cha mama yake alichotumia kujinyongea.
Mama Mzazi wa Marehmu akihojiwa na wandishi huku akiangua kilio.
Polisi wakiondoka eneo la tukio huku umati wawatu ulifuatilia tukio hilo la kusigitisha
Mwanafunzi wa wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mchikichini ‘B’ ya mjini hapa, Anosisye Gidion (12), ameacha viulizo kibao baada ya kujinyonga kwa kutumia kitenge cha mama yake, Judith Kilalu ‘Mama Kapipi’.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Ashura na rafiki wa marehemu, Hussein walisema kuwa chanzo cha denti huyo kujinyonga kilidaiwa kuwa ni kitendo cha mama yake kumchapa na kumtishia kumpeleka polisi baada ya kuchukizwa na kitendo chake cha kurudi nyumbani saa 6:00 usiku huku akidaiwa kuonekana akiwa na kundi haramu la vibaka la Kizazi Jeuri.
“Mwanangu alichelewa kurudi nyumbani usiku. Nilizunguka kumtafuta,
nikaambiwa alionekana akiwa na Kizazi Jeuri hivyo nilimchapa sana na kumtisha
kukicha nitampeleka polisi.
“Kulipokucha aliandaa nguo za shule, cha ajabu
nimemkuta amejinyonga. Inauma sana jamani.”amezungumza maam wa marehemu
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Makaburi B, Amiri Kombo
aliyekuwepo eneo la tukio alithibitisha kutokea kwa tukio hilo katika mtaa
wake.
Innalillah Wainalillah rajun.....
ReplyDelete