Mahakama ya wilaya ya Nyamagana,Mkoani Mwanza jana ilimhukumu miaka
miwili jela mzazi mwenzie na msanii Nay Wa Mitego, Siwema Edson kwa
makosa ya kimtandao,msanii huyo anafikiria kuahirihisha shoo yake kwa
mwisho wa mwezi huu ili aende Mwanza kumsaidia mama watoto wake huyo.
‘’Inabidi niondoke hivi karibuni ilibidi nisubiri nimalize shoo
lakini kwa ajili ya kumpambania kwa ajili ya kwenda kujua ‘situation’ ya
kule ikoje na pia wapi pa kuanzia,mwisho wa mwezi huu nina shoo mjini
Sumbawanga lakini inabidi niende kwanza Mwanza nikafight suala la huyu
bibie halafu nijue inakuwaje kama nita’cancel’ shoo au itakuwaje lakini
hadi sasa hivi nawasiliana na ndugu zake kila mtu amekuwa kama amepagawa
hivi hakuna anayejua wapi kwa kuanzia unajua kimekuwa ni kitu ambacho
hakuna mtu aliyekuwa anategemea’’Alisema Nay Wa Mitego.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment