Eneo hilo lililo chini ya ulinzi mkali kwa kuwa ni eneo lenye majengo ya serikali ikiwemo pia ubalozi.
Waandamanaji hao walikuwa wakidai mabadiliko katika muundo wa serikali hiyo baada ya kuwa na tetesi za ufisadi serikalini.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na shirika la habari la Al Jazeera ni kuwa watu hao waliokuwa wakiandamana walipasua ukuta kwa kutumia nyaya.
Ghasia hizo za maandamano zimetokea baada ya wabunge kushindwa kuidhinisha kufutwa kazi kwa baadhi ya mawaziri wanaoshutumiwa kushiriki rushwa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment