April 01, 2016


Hofu imezuka kwa wakazi wa kijiji cha Manchali, wilayani Chamwino mkoani Dodoma baada ya mama mmoja aliyetambulika kwa jina la Joyce Elias kujifungua mtoto wa ajabu akiwa na uzito usio wa kawaida wa kilo 4 na gramu 900 huku kichwa chake kikiwa ni kidogo chenye uwazi sehemu ya utosini na kuitaka serikali kutuma wataalam wa afya kuchunguza tatizo hilo wakidai linafanana na viashiria vya ugonjwa wa homa ya zika.
Mtoto huyo aliyezaliwa katika kijiji cha Manchali alfajiri ya siku ya alhamis tarehe 31 march mwaka huu na taarifa zake zikizua taharuki kwa wakazi wa eneo hilo ambapo Mganga wa zahanati ya Manchali Gaudensia Mpokwa amesema wameshindwa kutambua mara moja tatizo la mtoto huyo.
 
Tukio hilo linalodaiwa kuwa ni la kipekee katika eneo kijiji hicho licha ya kuwepo kwa matukio mengi ya watoto kuzaliwa na maumbile yasiyo ya kawaida yanadaiwa kuchagizwa kwa kiasi kikubwa na kinamama wengi kutohudhuria kliniki wakati wa ujauzito. 
 
Kufuatia kuzuka kwa hofu hiyo Kaimu Mganga Mkuu wa Dodoma Dr. Nasoro Mzee amesema utafiti wa kitaalam pekee ndio unaweza kutoa majibu kama ni homa ya zika lakini akaeleza kuwa hali hiyo pia hutokea kutokana na kukosekana kwa baadhi ya vitamini kwa mama wakati wa ujauzito

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE