
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amewaagiza wa
wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha kuwa viwanja vya michezo vilivyo
vamiwa na kujengwa vina kuwa wazi ndani ya siku 30.
Nnauye ametoa
agizo hilo mkoani Geita jana wakati akizungumza na wasanii ,maofisa
utamaduni wa mkoa, maofisa habari, wanahabari, wanamichezo, wadau wa
soka pamoja na kamati ya ulinzi na usalaama wilaya ya Geita.
Amesema
kuwa wakuu hao wanatakiwa kuhakikisha viwanja hivyo vinakuwa wazi
ndani ya siku 30 ili viwanja hivyo viweze kutumiwa na wanamichezo kwa
malengo yaliyo kusudiwa na kuibua vipaji kwa vijana na kuwataka watoe
taarifa za viwanja hivyo .
”Wakuu
wa mikoa na wilaya hakikisheni mnafuatilia viwanja hivyo vina kuwa
wazi ndani ya siku 30 na mnitumie taarifa kwa kila
hatua,” amesema Nnauye.
Pia
amezitaka halmashauri nchini kuwa ajiri maofisa habari pamoja na
kuwapa nafasi ya kushiriki katika vikao vya maamuzi katika halmashauri
zao ili waweze kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari ili kuepusha
wanahabari kuandika habari zisizo sahihi kutokana na kutopewa
ushirikiano.
Awali
kaimu mkuu wa mkoa wa Geita, Manzie Omary Mangochie akisoma taarifa ya
mkoa wa Geita amesema kuwa mkoa huo unakabiliwa na changamoto lukuki
katika sekta hiyo ikiwemo ukosefu wa viwanja vya michezo ,watalaamu wa
michezo .
Alphonce Kabilondo na Cassimili Mbasa ,Geita
0 MAONI YAKO:
Post a Comment