May 04, 2016

BEI ya sukari yaendelea kuwa kizungukuti kutokana na kutokuwepo bei sahihi licha ya serikali kutoa bei elekezi ya 1,800 TZS huku maagizo ya viongozi wa ngazi ya juu yakigonga mwamba kutokana na kuwaeleza wananchi kuwa sukari ipo ya kutosha jambo ambalo limekuwa kinyume kutokana na sukari hiyo kutopatikana kwa uhakika mkoani Kagera.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji Charse Mwijage siku chache zilizopita akiwa katika kiwanda cha kuzalisha sukari (Kagera Sugar) na kuwaaminisha watanzania kuwa sukari ipo ya kutosha nchini.
Lakini pia hivi karibuni waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa akiwa katika ziara yake mkoani Kagera alitembelea kiwanda hicho na kushuhudia uzalishaji wa sukari ambapo alisema kuwa serikali haina haja ya kuagiza asukari kutoka nje ya nchi.
Kauli hizo za viongozi hao wa serikali zinakuwa kinyume kwa sasa baada ya ya wananchi kuanza kununua sukari kwa bei ya shilingi elfu 2,400 TZS hadi elfu 2,700 TZS huku wengine wakiinunua kwenye maduka maalumu ambayo yamepangwa na uongozi wa ngazi ya mkoa.
Clouds TV imefanikiwa kuongea na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misenyi ambapo amesema kuwa,wao hawaoni umuhimu wa kiwanda cha Kagera Sugar licha ya kuwa katika halmashauri hiyo kutokana na kuwepo mfumuko wa bei ya sukari mkoani Kagera.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE