May 30, 2016

13108612_1134282759961344_2144088758_n
 Raymond ni msanii mwenye vipaji vingi vilivyomvutia Diamond amsainishe kwenye label yake, WCB.
Miongoni mwa vipaji alivyonavyo ni uandishi wa nyimbo huku akiwa ameshiriki kuandika hits kadhaa zikiwemo za bosi wake, Diamond. Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, Ray alisema bosi wake ni mtu anayependa sana kushauriana na watu mbalimbali ili kupata kitu kizuri na ndio maana alimpa nafasi kijana wake ampe melody na mistari kadhaa kwenye verse ya remix ya Zigo ya AY.
“Yeye ni msanii wa melody za kulalamika sana kwahiyo alivyosikia ile beat ina uchizi flani, kuna baadhi ya melody kama ile mukide mukide nikamuambia tukiweka hapa inakaaje, yeye anatafuta maneno,” alisema Ray.
Amesema pia alishiriki kutoa idea zake kwenye Make Me Sing. Lakini amedai kuwa bosi wake pia ameshiriki kumpa maneno mengi na melody kwenye wimbo wake Kwetu. Pia amedai kuwa Harmonize naye amechangia ideas zake kwenye wimbo wake Natafuta Kiki.
Kwa upande mwingine Ray alishirikiana an Dogo Janja kuandika wimbo wake My Life.
Akizungumzia boss wake, Ray amesema Diamond ni msanii anayeishi maisha simple kuliko watu wanavyoweza kudhani.
Msikilize zaidi hapo chini.


0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE