Msanii
Madee amefunguka undani wa wimbo wa 'Haya Yote Maisha' wa Producer P
Funk Majani ambao ameimba yeye, wimbo ambao ulishika chati na kugusa
hisia za watu wengi.
Akiongea
kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Madee amesema wimbo huo ni
historia ya kweli ya P Funk na mwanamke ambaye ndiye mama wa mtoto wake
wa kwanza, Kajala Masanja.
“Haya
yote maisha imetokea kipindi ambacho bado nipo na P Funk, alafu P Funk
ana matatizo na mama mtoto wake Kajala, kwa hiyo wakati mi naenda pale
kurekodi cheza kidogo, kabla sijamalizana na ile nakutana na beat ya
yote maisha inaplay, alafu inaplay na chorus lakini hakuna verse, lakini
the way ile beat inavyoplay majani anavyoiimba anaimba kwa feelings
kinoma, nikamwambia bwana hii nyimbo mbona kali nigaie niimbe akasema
hii na chana mwenyewe babu,” alisema Madee.
Madee aliendelea kusema baada ya
mazungumzo P Funk alikubali kumpa beat na kwenda kuifanyia kazi, baada
ya kukumbuka Madee mtindo alioutumia kwenye nyimbo zake.
“Sema wewe ulivyochana kwenye kazi
yake mola kuna ryhmes fulani naona unapita pita, unaongea kimajonzi
hebu chukua hii beat kaandike, kwa hiyo nikapewa ile beat, aliniambia
kwamba hii nyimbo ina feeling zangu, nataka uandike kitu hiki na hiki,
kwa hiyo idea iliyotoka mule ni idea ya P Funk,” alisema Madee
akimuongelea P Funk Majani.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment