Kwa
kutambua uwezo walionao watoto katika kubuni vitu mbalimbali, Taasisi
ya XPRIZE iliyo na makazi yake nchini Marekani, imezindua mradi wa
XPRIZE nchini ambao utahusisha watoto ambao hawapo shuleni ukiwa na
malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa kutumia uwezo walionao watoto
wa miaka 5-12.
Akielezea mradi huo, Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, alisema
kuwa wameanzisha mradi huo kwa kutambua uwezo ambao wanao watoto na
kama wakiwezeshwa wanauwezo wa kufanya mambo makubwa.
Alisema
dunia ina watoto wengi ambao hawapo shuleni kwa sababu mbalimbali na
hivyo mradi huo utakwenda kufanyika kupitia watoto ambao hawapo
mashuleni na watawapatia vifaa mbalimbali ili waweze kupimwa uwezo wao
katika kazi zinazohusiana na teknolojia.
“Dunia
ina watoto Milioni 57 ambao hawapo shuleni tutawatumia kama hao kwa
sababu tunaamini watoto wanaweza kufanya mambo mengi lakini
wanachohitaji ni kuwezeshwa ili waweze kukamilisha mambo wanayofanya,”
alisema Keller.
Nae
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira
Rodrigues alisema kuwa ni muda muafaka kwa watoto kusaidiwa kupata elimu
kwa njia ya kiteknolojia hasa kwa wakati uliopo ambao teknolojia
inatumika zaidi katika kurahisisha kazi mbalimbali.
Alisema
ni muhimu kwa Tanzania kuanza kutumia mifumo ya teknolojia hasa katika
kipindi hiki ambacho nchi ipo katika hatua za kuelekea uchumi wa kati
kwani kwa kufanya hivyo itaweza kurahisha kufikiwa malengo kwa muda
muafaka ambao umepangwa.
“Ni
wakati kwa watoto kupata elimu ya teknolojia, haijalishi hayupo shuleni
kwa kipindi hiki teknolojia inatumika zaidi na hii itasaidia wakati huu
ambao nchi (Tanzania) inakwenda katika uchumi wa kati,” alisema Bi.
Rodrigues.
Nae
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi,
Prof. Simon Msanjila alisema kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada
mbalimbali ili kuwawezesha watoto kupata elimu ya teknolojia lakini
inakuwa ni ngumu kufikia malengo hayo yenyewe hivyo ni tumaini lao mradi
huo utafanikiwa.
Alisema
ni muhimu kwa watoto kupatiwa elimu ya teknolojia kwa dunia ya sasa na
serikali ipo tayari kushirikiana nao kwa pamoja ili mradi huo uweze
kufanyika kama jinsi umevyopangwa na Taasisi ya XPRIZE ambao ndiyo
waanzilishi wa mradi huo ambao unataraji pia kufanyika nchi mbalimbali
duniani.
“Unaposema
dunia inakuwa kijiji ina maana unazungumza kuhusu teknolojia kutokana
na kusogeza kila jambo karibu na kwa haraka ni ngumu kwa serikali
kufanya yenyewe lakini wanapopattikana watu wanaosaidia inakuwa vizuri
na pia inasaidia kukuza teknolojia nchini,” alisema Prof. Msanjila.
Nae
Afisa Mradi wa Elimu wa UNESCO, Faith Shayo alisema mradi huo nchini
utaanza kwa majaribio katika makundi 200 kutoka mkoa wa Tanga katika
wilaya ya Lushoro, Korogwe, Muheza, Pangani, Mkinga, Handeni na Kilindi
na mkoa wa Arusha utafanyika katika wilaya ya Ngorongoro ambapo watoto
hao watapatiwa simu zilizo na muundo wa tablet na sola za kuchajia na
watatumia ‘tablet’ kwa kusoma, kuandika na kuhesabu na baada ya hapo
watakuwa wakichaguliwa kutokana na uwezo binafsi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa
Simon Msanjila (kulia) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mradi wa kukuza
teknolojia kupitia watoto XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa
wiki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka
Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim
Kaoneka na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira
Rodrigues.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues
akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa XPRIZE uliofanyika
mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya
Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), Kassim Kaoneka. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Simon Msanjila.
Naibu
wa Programu kutoka Shirika la Chakula Duniani (WFP) nchini, Marina
Negroponte (kulia) akizungumzia nafasi ya Shirika lake katika
utekelezaji wa mradi wa XPRIZE katika hafla fupi ya uzinduzi wa mradi
huo iliyofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Pichani
juu na chini ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Mafunzo kutoka Taasisi ya
XPRIZE, Matt Keller akizungumzia malengo ya mradi huo wakati wa hafla
fupi ya uzinduzi iliyofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Makamu
wa Rais anayeshughulikia uendeshaji wa XPRIZE Foundation, Joel Carnes
akifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi wa mradi huo uliofanyika
mjini Dodoma, mwishoni mwa wiki.
Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Ufundi, Profesa Simon S. Msanjila (kushoto) akijadili jambo na Mkurugenzi
wa Elimu ya Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Ufundi, Sarah Mlaki wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kukuza
teknolojia kupitia watoto XPRIZE uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini
Dodoma.
Kutoka
kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira
Rodrigues, Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka, Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Simon
Msanjila wakifuatilia kwa umakini ‘power point presentation’ ya jinsi
mradi huo utakavyotekelezeka nchini.
Afisa
Mradi wa Elimu wa UNESCO, Faith Shayo akizungumzia utekelezaji wa mradi
huo wa kukuza teknolojia kupitia watoto XPRIZE na wadau
watakaoshirikiana nao katika kutekeleza.
Kutoka
kushoto ni Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka, Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Simon
Msanjila, Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi, Sarah Mlaki, waandishi wa habari pamoja na wadau
wa sekta elimu waliohudhuria uzinduzi huo, mjini Dodoma mwishoni mwa
wiki.
Naibu
wa Programu wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) nchini, Marina
Negroponte akiandika mambo muhimu kwenye uzinduzi wa mradi wa XPRIZE.
Afisa
mradi wa Elimu wa Unesco, Dar es Salaam, Faith Shayo akijadiliana jambo
na Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt
Keller wakati wa uzinduzi wa mradi wa XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma
mwishoni mwa wiki.
Baadhi
ya wadau wa sekta ya elimu, waandishi wa habari na viongozi kutoka
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi waliohudhuria uzinduzi
huo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Hoteli ya Veta, mjini
Dodoma.
Baadhi ya wageni waalikwa wakibadilishana mawazo kwenye uzinduzi wa mradi wa XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Ufundi, Profesa Simon Msanjila akiagana na Mkurugenzi Mwandamizi wa
Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller….Kulia Mkuu wa Ofisi
na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues na kushoto
ni Makamu wa Rais anayeshughulikia uendeshaji wa XPRIZE Foundation, Joel
Carnes.
Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Ufundi, Profesa Simon Msanjila akizungumza na waandishi wa habari nje ya
ukumbi wa mikutano wa Veta mara baada ya kuzindua rasmi mradi huo.
Mkurugenzi
Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller
(katikati) akizungumza na mmoja wa waandishi wa habari nje ya ukumbi wa
Veta mjini Dodoma, mara baada ya uzinduzi wa mradi huo. Kulia ni Makamu
wa Rais anayeshughulikia uendeshaji wa XPRIZE Foundation, Joel Carnes.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment