May 26, 2016





wp-1464124105944.jpeg
Msanii wa filamu Jacqueline Wolper ameweka wazi jinsi yalivyoanza mahusiano yake ya mapenzi na hit maker wa wimbo ‘Bado’ Harmonize kutoka WCB.
Akizungumza Jumatano hii katika kipindi cha Take One Cha Clouds TV, Wolper amesema alitokewa na Harmonize wakati sahihi ambapo ameshaachana na mkongo wake ambaye alivyalisha pete.
“Rajabu (Harmonize) sijamjua hivi karibuni, nimemjua siku nyingi sana na nilikuwa namchukulia kama wasanii wengine wa muziki,” alisema Wopler.
“Lakini kwa mimi nilikuja kugundua Rajabu alikuwa ananikubali siku nyingi, tukawa marafiki. Lakini katika kumbukumbu zangu na vitu ambavyo nimevipitia, naamini kwamba Rajabu alikuwa anashindwa kuniambia. Lakini alikuja kunitamkia mimi wakati nipo kwenye wakati mgumu sana, kwa hiyo tukajikuta kunakuwa marafiki na baadae wapenzi,” aliongeza.
Wopler amesema ana mwezi mmoja na wiki mbili toka aingie rasmi kwenye mahusiano ya mapenzi na Harmonize.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE