Mamlaka ya chakula na Dawa TFDA kanda ya ziwa, imelifunga na
kulifutia leseni Duka la dawa la Get well Medics lililopo Igoma mkoani
Mwanza kwa kukutwa likiuza na kutengeneza juisi badala ya kuuza Madawa
Baridi. Mkaguzi wa TFDA kanda ya ziwa amesema wameamua kulifungia Duka hilo
baada ya kukutwa likiuza na kupakia juisi kinyume cha Sheria. Taarifa Zaidi zinasema kuwa mmiliki wa kiwanda hicho bubu alitumua mbio za haja akihofia kukutana na mkono wa Sheria. Mkaguzi huyo amekiri kukutwa chupa 470 zilizojazwa juisi aina ya ‘Poa
Fruit Drink’ na chupa zingine 300 tupo zikisubiri hatua ya kujazwa
kinywaji hicho.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment