Timu ya kimataifa ya wanasayansi
imekamilisha utafiti mkubwa zaidi kuwahi kutokea wa maumbile ya saratani
ya matiti, ambayo wanasema inawapa karibu picha kamili ya nini
husababisha ugonjwa huo.
Wanasayansi hao wanajaribu kutizama
mfuatano wa jinomu kamili wa kesi zaidi ya mia tano za saratani ya
matiti.Utafiti huo unaoongozwa na taasisi ya Cambridge umeweza kugundua
aina tano mpya za visababishi (seli) vya ugonjwa huo.Utafutu huo walau unaweka wazi uhakika wa asilimia 93 kama seli hizi zikibadilika kuweza kusababisha uvimbe.Watafiti wanasema kuwa taarifa hizi zitaweza kusababisha kupatikana matibabu kamili kwa binadamu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment