May 31, 2016

 Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo na kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe, amemtolea uvivu rais Magufuli na kuandika hiki katika AC yake ya Facebook

"Rais Magufuli tunakuunga mkono kwa dhati kupambana dhidi ya ufisadi. Tunakupinga kwa nguvu zote kupambana dhidi ya demokrasia.
Kuanzia mwanzo tumekuunga mkono dhidi ya ukwepaji kodi, ubadhirifu, uvivu na uzembe. Tangia mwanzo tulionya kuwa ni lazima udhibitiwe na Bunge ili ufanye kazi kwa mujibu wa Katiba. Hivi sasa wewe Rais ndio unaendesha Bunge kwa remote control. Tutakupinga kuturudisha nyuma. Hutafanikiwa kamwe kubomoa misingi ya taasisi za uwajibikaji tulizoanza kuzijenga.
Narudia nukuu muhimu sana " ukitaka kutawala tawala peke yako. Ukitaka kuongoza ongoza na wenzako". Rais Magufuli Tanzania inataka Uongozi madhubuti na sio utawala wa imla. Huko tumeshatoka na Watanzania hawatakubali kurudi huko".

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE