Raia
mmoja anakabiliwa na mashataka baada ya kutuhumiwa kuandika ujumbe
kwenye mtandao whatsApp akimuita Rais Magufuli mpumbavu, Bwege, Zuzu.
Mtu huyo aliyefahamika kwa jina la
Leonaard Mulokozi Kyaruzi ameshtakiwa chini sheria uhalifu wa mtandaoni
(Cybercrime act) ya mwaka 2015. Huyu ni raia wa pili kushtakiwa baada ya
wa kwanza kufikishwa mahakamani mkoani Arusha kwa kumtukana Rais
Magufuli kwenye mtandao wa Facebook.
Kyaruzi ujumbe wake unasomeka hivi. ‘Hivi
huyu Pombe ni kwamba hana washauri? Hashauri? Au ni zuzu? Bwege sana
huyu jamaa, he doesn’t consider the law in place before opening his
mouth!. Au na yeye anaumwa ugonwja wa mnyika?”
Hii hapa ni hati ya shtaka linalomkabili Kyaruzi.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment