
Mgombea urais wa chama cha
Republican nchini Marekani Donald Trump amemsifu kiongozi wa zamani wa
Iraq Saddam Hussein akisema aliweza kukabiliana vyema na magaidi.
Bw
Trump alikuwa akihutubia mkutano wa kampeni eneo jimbo la North
Carolina Jumanne alioanza kuzungumza kuhusu kiongozi huyo aliyeuawa kwa
kunyongwa Desemba 2006.“Saddam Hussein alikuwa mbaya, kweli? … Lakini mnafahamu ni jambo gani aliweza kulifanya vyema sana? Aliwaua magaidi. Alifanya hivyo vyema sana,” Trump alisema.
“Hawakuwasomea haki zao, hawakunena lolote. Walikuwa magaidi, mambo yao kwisha.”
Bw Trump awali amewahi kusema kwamba ulimwengu ungelikuwa “asilimia 100 bora kuliko sasa” iwapo viongozi wa kiimla kama Saddam Hussein na kiongozi wa muda mrefu wa Libya Muammar Gaddafi wangelikuwa bado uongozini.
Kabla ya uvamizi ulioongozwa na Marekani, ambapo Saddam aliondolewa madarakani, Iraq ilikuwa imeorodheshwa na Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani kama taifa linalofadhili ugaidi.
Donald Trump pia aliwahi kusema kuwa dunia ingekuwa mahala salama zaidi kama tu Saddam Hussein wa Iraq na Maummar Gaddafi wa Libya wangelikuwa hai.
Afisa mkuu mshauri wa Hillary Clinton kuhusu sera, amejibu matamshi ya Bw Trump kwa kusema kuwa: “Sifa za Donald Trump kwa viongozi wa kiimla yamkini hazina mipaka.”
Amesema matamshi kama hayo yanaashiria “ni jinsi gani itakuwa hatari (kuwa na Trump) kuwa Amiri Jeshi Mkuu na jinsi ambavyo hafai kuhudumu kama rais.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment