July 14, 2016

fiesta

fiesta
( Pichani ni Mkurugenzi wa Prime Time Promotions @josephkusaga akipeana mkono na Afisa Biashara Mkuu wa Tigo , Shavkat Berdiev. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fiesta , @sebamaganga (kushoto) na Katibu Mtendaji wa BASATA , Ndugu Godfrey Ngereza )
Tamasha la Fiesta 2016 limezinduliwa leo rasmi na waandaji Prime Time Promotion na wadhamini wakuu wa Tamasha hilo mwaka huu kampuni ya simu ya Tigo, Fiesta 2016, itafanyika katika mikoa 15 Tanzania na pazia litafunguliwa rasmi ndani ya Rock City – Mwanza.
Kampuni ya simu ya Tigo wametangaza rasmi kushirikiana na Prime Time Promotions kudhamini Tamasha la ‪‎Fiesta2016.
fiesta3
Naye Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga alisema kuwa Fiesta kwa mwaka huu itaanza katika wiki ya tatu ya mwezi wa nane na kuhusu suala la muda wa kuisha watawajulisha kadri ya wakati. 

fiesta1 

‘’Tunatarajia mwaka huu Fiesta itaanza katika wiki ya tatu ya mwezi wa nane kuhusu suala la muda wa kuisha tutawajulisha kadri ya wakati’’. Alisema Joseph Kusaga.

fiesta2
Naye mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Fiesta, Seba Maganga alisema ‘’Shughuli za awali zitakazokuwepo katika Tamasha la mwaka huu kama kawaida tutakuwa na Fiesta Tamadunika ambayo itajumuisha shughuli za Fursa, Michakato inaendelea kuhusu msanii gani atakuja kutoka nje tutawajulisha kadri ya wakati ndugu waandishi’’.

IMG-20160714-WA0067

Related Posts:

1 comment:

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE