August 20, 2016

 HATIMAYE mwili wa mwimbaji mkongwe wa taarab Tatu Said maarufu kama Shakila Said umehifadhiwa katika nyumba yake ya milele leo saa 10 alasiri. Mazishi ya Bi Shakila aliyefariki jana usiku, yamefanyika katika makaburi ya Charambe, jijini Dar es Salaam mwendo mfupi kutoka nyumbani kwake. Makamu wa Rais mama Samia Suluhu aliongoza mamia ya waombolezaji waliofika nyumbani kwa marehemu Shakila ambaye alifariki ghafla baada ya kudondoka muda mfupi baada ya kupata sala ya magharibi. Aidha, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye naye alikuwepo msibani na akaongoza waombolezaji wa kiume kuelekea makaburiki kumzika Bi Shakila kwa taraibu zote za dini ya Kiislam. Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano Dr. Jakaya Kikwete yeye alipitiliza moja kwa moja makaburini kushiriki mazishi kabla ya kwenda nyumbani kwa Bi Shakila kujumuika na wafiwa na kuwapa pole. Kikwete alibadilisha hali ya hewa nyumbani kwa marehemu kwa hamasa ya aina yake na ya kusisimua baada ya waombolezaji kumshangilia kwa nguvu mara tu aliposhuka kwenye gari lake na kuanza kutembea kwa mguu. Kwa sekunde kadhaa ni kama vile waombolezaji waliusahau msiba kwa faraja ya kumuona rais mstaafu. Pata picha za mazishi ya Bi Shakira hapa















HATIMAYE mwili wa mwimbaji mkongwe wa taarab Tatu Said maarufu kama Shakila Said umehifadhiwa katika nyumba yake ya milele leo saa 10 alasiri. Mazishi ya Bi Shakila aliyefariki jana usiku, yamefanyika katika makaburi ya Charambe, jijini Dar es Salaam mwendo mfupi kutoka nyumbani kwake. Makamu wa Rais mama Samia Suluhu aliongoza mamia ya waombolezaji waliofika nyumbani kwa marehemu Shakila ambaye alifariki ghafla baada ya kudondoka muda mfupi baada ya kupata sala ya magharibi. Aidha, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye naye alikuwepo msibani na akaongoza waombolezaji wa kiume kuelekea makaburiki kumzika Bi Shakila kwa taraibu zote za dini ya Kiislam. Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano Dr. Jakaya Kikwete yeye alipitiliza moja kwa moja makaburini kushiriki mazishi kabla ya kwenda nyumbani kwa Bi Shakila kujumuika na wafiwa na kuwapa pole. Kikwete alibadilisha hali ya hewa nyumbani kwa marehemu kwa hamasa ya aina yake na ya kusisimua baada ya waombolezaji kumshangilia kwa nguvu mara tu aliposhuka kwenye gari lake na kuanza kutembea kwa mguu. Kwa sekunde kadhaa ni kama vile waombolezaji waliusahau msiba kwa faraja ya kumuona rais mstaafu. Pata picha 35 za mazishi ya Bi Shakila kuanzia nyumbani kwake hadi makaburini.

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/08/picha-35-rais-mstaafu-jakaya-kikwete.html#more
Copyright © saluti5

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE