August 21, 2016

CHAMA cha Wananchi (Cuf) leo kinatarajia kumpata mrithi wa Profesa Ibrahim Lipumba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho, baada ya kufanyika mkutano na Uchaguzi Mkuu kwa ajili ya kuchagua viongozi katika nafasi mbalimbali.

Profesa Lipumba aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, alitangaza kujiuzulu uenyekiti kwa madai ya kutoridhishwa na baadhi ya mambo ikiwemo Umoja wa Ukawa kumteua Edward Lowassa kuwa mgombea wake wa urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Mkutano Mkuu huo unafanyika leo baada ya vikao vya Kamati Kuu ya Utendaji na Baraza Kuu la chama hicho kuchambua na kuchagua majina matatu kati ya tisa ya wanachama waliojitokeza kuwania nafasi hiyo na majina mengine manne ya waliojitokeza kuwaia nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

Shemu ya taarifa ya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Salim Bimani, ilisema, “Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Taifa na Baraza Kuu la Uongozi kimefanyika leo (jana), kimechambua na kufanya mapendekezo juu ya majina yatakayowaslihwa kesho (leo) na kamati ya utendaji ya ta

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE