Waziri wa maswala ya kigeni nchini
Marekani John Kerry ameitaka Sudan Kusini kuwakubali wanajeshi 4000 wa
Umoja wa Mataifa nchini humo.
Akizungumza baada ya kukutana na
rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mawaziri wa maswala ya kigeni jijini
Nairobi,Kerry amesema kuwa Sudan Kusini inafaa kuheshimu makubaliano ya
amani nchini humo kwa maneno na vitendo ili kuhakikisha kuwa
yanaafikiwa.
Amewataka viongozi wa taifa hilo kutojihusisha na vitendo vya ghasia ambavyo vinaweza kuchangia vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mapema mwezi huu Sudan Kusini ilisema kuwa haitashirikiana na Umoja wa Mataifa .
Bwana Kerry pia amesema kuwa mafanikio makubwa yameafikiwa katika
kukabiliiana na tishio la wapiganaji wa kundi la al-Shabab nchini
Somalia,lakini mengi yanahitajika kufanywa katika eneo hili.
Ameongezea kuwa Marekani itaahidi dola milioni 138 za misaada ya kibinaadamu kwa Sudan Kusini mwaka huu.
Ameongezea kuwa Marekani itaahidi dola milioni 138 za misaada ya kibinaadamu kwa Sudan Kusini mwaka huu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment