Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17 inatarajiwa kuanza kesho
Jumamosi Agosti 20, 2016 kwa michezo mitano huku Bingwa Mtetezi wa Kombe
hilo 2015/16, Young Africans ya Dar es Salaam ikisubiri hadi Agosti 31,
2016 kuanza kutetea taji lake.
Young
Africans inatarajiwa kusafiri kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC), kucheza na TP Mazembe kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho
unaotarajiwa kufanyika Agosti 23, mwaka huu.
Michezo
itakayochezwa kesho ni pamoja na Simba SC itakayoikaribisha Ndanda FC
ya Mtwara kwenye Uwanja wa Taifa, ulioko Chang’ombe Dar es Salaam,
katika mchezo utakaoanza saa 10.00 jioni wakati Azam itakuwa mwenyeji wa
African Lyon kwenye Uwanja wa Azam FC ulioko Chamazi-Mbagala, nje
kidogo ya jiji.
Kadhalika
Stand United ya Shinyanga itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye
Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga sawa na Mtibwa Sugar
itakayoikaribisha Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa Manungu
uliuoko Turiani, Mvomero mkoani Morogoro wakati Prisons ya Mbeya
itasafiri hadi Uwanja wa Majimaji ya Songea kucheza na Majimaji FC ya
huko.
Wakati
ligi ikianza, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaonya timu
kuchezesha wachezaji wa kigeni kama hawana vibali vya kuishi, kufanya
kazi na leseni inayomruhusu kucheza ligi husika kwa mujibu wa sheria za
nchi na kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Vibali vya kuishi
na kufanya kazi vinatolewa na Idara ya Uhamiaji Tanzania (Uhamiaji)
wakati leseni ya kucheza inatolewa na TFF. Vilevile tumeziagiza klabu
kulipia ada za ushiriki kwa kila timu; leseni za wachezaji, ada za
wachezaji na ada za mikataba. Mchezaji hatapewa leseni ya kucheza kama
uongozi wa timu hautakamilisha taratibu za malipo.
TFF
linapenda kuzikumbusha timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara kwamba hatutatoa leseni ya mchezaji yeyote ambaye timu haikuleta
mkataba wakati wa maombi ya usajili, hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 68
vipengele vya 1, 2, 3 na 8 ya Ligi Kuu ya Tanzania toleo la 2016/2017.
Kila
timu inatakiwa kuleta nakala tatu za mkataba wa mchezaji, ili kamati ya
katiba, sheria na hadhi za wachezaji iweze kupitia na TFF iweze
kuidhinisha mikataba hiyo. Baada ya hapo timu na mchezaji, watakuja
kuchukulia mikataba hiyo hapa TFF. Ni matarajio yetu kuwa kila klabu
itatimiza wajibu wake ili kuondoa migogoro kati ya timu na mchezaji na
mchezaji na timu. Tunategemea kupata ushirikiano.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment