Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imewataka wafanyabiashara katika jiji
la Dar es salaam kuboresha taarifa za usajili wa namba ya utambulisho wa
mlipa kodi (TIN) ili kuondokana na mfumo wa kizamani wa usajili wa
namba hiyo.
Uhakiki huo utaiwezesha mamlaka hiyo kuweza kujua idadi sahihi ya
wafanyabiashara walipa kodi, kuondoa walipa kodi hewa ambao wamekuwa
hawajihusishi na biashara kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo au
kufungwa kwa makampuni yao.
Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ndugu Alphayo Kidata amesema mfumo
huo utawawezesha wafanyabi
Kidata amesema kuwa mfumo wa sasa wa uhifadhi kumbukumbu za walipa kodi
ulikuwa na kasoro nyingi hivyo mfumo mpya utaendana na ukuaji wa
teknolojia na kukuza uchumi.
“Zoezi hili linamtaka kila mwenye namba ya utambulisho yani TIN kufika katika ofisi za TRA zilizopo karibu naye bila kuwakilishwa na mtu yeyote na zoezi litatumia dakika 10 kumalizika” amesema
Naye Elija Mwandubya ambaye ni kamisha wa mapato wa ndani wa mamlaka hiyo, amesema zoezi hilo litachukua siku 60 na kuanzia Dar es salaam na baadaye kuhamia mikoa mingine ndani ya nchi.
“TRA ina wafanyabiashara walipa kodi milioni mbili na laki moja hivyo uboreshwaji wa TIN utatupa uelewa wa idadi kamili ya walipa kodi” Amesema
Elija amesema kutakuwa na vituo maalum kwaajili ya uhakiki wa taarifa katika mikoa ya kikodi ambapo Kinondoni wafanyabiashara watatakiwa kutembelea ofisi za TRA zilizopo jengo la LAPF – Kijitonyama na Kibo Complex Tegeta.
Ilala wafanyabiashara watembelee ofisi ya TRA shauri moyo na 14 Rays Gerezani na Temeke wafike ofisi za uwanja wa Taifa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment