Polisi nchini
Burundi wamewatia nguvuni wajumbe wanane wa mtandao wa kijamii wa
WhatApp . Kulingana na msemaji wa wizara ya usalama wa umma nchini humo
Pierre Nkurikiye watu hao ambao ni wakazi wa mji mkuu Bujumbura
walikamatwa mnamo tarehe 20 Agosti kutokana na "vitendo vya uhalifu wa
kimtandao ".
Wanane hao kwa pamoja walikuwa ni wajumbe wa kundi moja la WhatsApp. Kwa mujibu wa Nkurikiye WhatsApp mijadala inayoendelea katika makundi ya WhatsApp inaeneza taarifa za "matusi ni chanzo cha ghasia nchini humo hasa wakati wa hali ya sintofahamu".
Mkuu wa uchunguzi wa habari Innocent Muhozi ameishutumu serikali kwa kujaribu " kukamilisha njama yake ya kuzima uhuru wa mawasiliano" waliyoianzisha kwa kuwakamata watumiaji wa WhatsApp.
Muhozi anasema mtandao huo ulikua ndio chanzo cha taarifa huru kilichobaki kwa warundi .
Wakazi wa Bujumbura hutumia WhatsApp kila siku kama mfumo wa kutoa tahadhari baina yao kuhusu utekeji nyara, kamata kamata ya maafisa wa usalama na kutoweka na matukio ya uhalifu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment