Iraq imewanyonga
wapiganaji 36 wa kundi la Islamic State wanaohusishwa na mauaji ya
makurutu 1,700 katika kambi moja iliokuwa ya Marekani mwaka 2014.
Mauaji
hayo katika kambi ya Speicher karibu na Tikrit yalifanywa na wapiganaji
kutoka Islamic State ilipochukua udhibiti wa eneo la kaskazini mwa
Iraq.
Hisia kali zilizotolewa kufuatia mauaji hayo ya raia wa
Kishia zilichochea kubuniwa kwa kundi la wapiganaji wa Kishia katika
vita dhidi ya Islamic State.
Wapiganaji wa Islamic State walitoa picha na video wakionyesha mauaji hayo ya 2014.
Makaburi ya halaiki yalifichuliwa mwaka mmoja baadaye.
Makaburi hayo yaligunduliwa baada ya wanajeshi wa Iraq kulikomboa eneo hilo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment