Yanga na Azam FC zinatarajiwa kukutana kesho Jumatano katika mechi ya
Ngao ya Hisani ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara msimu wa
2016/17, tayari kila upande unaonekana kuwa tayari.
Kila upande unaonekana kuwa fiti kwa mchezo huo japokuwa Yanga itakuwa
na wachezaji kadhaa majeruhi ambao watakosekana katika mchezo huo baadhi
yao ni Geofrey Mwashiuya, Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’
Yanga ambao upande wa uongozi kwa sasa hakujatulia kutokana na taarifa
za mwenyekiti wao, Yusuf Manji kutaka kujiuzulu nafasi hiyo, kikosi chao
kipo kwenye mazoezi katika Uwanja wa Gymkhan jijini Dar es Salaam
wakati Azam FC wao wapo kwenye Uwanja wao wa Azam Complex nje kidogo ya
Dar es Salaam.
Timu hizo ambazo katika miaka ya hivi karibuni zimekuwa na ushindani
mkali zitakutana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar kutokana na Yanga
kuwa bingwa wa Ligi kuu Bara wakati Azam ilishika nafasi ya pili katika
Kombe la FA, hivyo kwa kuwa kanuni inataka bingwa wa FA na ligi kuu
kukutana ilibidi Yanga icheze na Azam kwa kuwa Yanga pia ilichukua
ubingwa wa FA.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment