Zanzibar kwa wenye fedha zao huweza kugeuka kuwa paradise
iliyo chini ya jua. Kwa Diamond, Zanzibar imekuwa ni sehemu muhimu pindi
anapotaka kumpeleka mapumzikoni mchumba wake, Zari.
Kwa dhoruba kadhaa zilizojaribu kulipiga pendo lao miezi ya hivi
karibuni, mapumziko katika fukwe za visiwani humo zenye ukijani
unaovutia na upepo mwanana wa bahari ya Hindi, kilikuwa ni kitu
walichokihitaji zaidi.
Isitoshe, Zari amesherehekea siku yake ya kuzaliwa siku mbili hizi –
siku ambayo imemkuta akiwa amejaa, mimba nyingine, ya mtoto mwingine wa
kipenzi chake, Diamond. Ni zawadi gani nyingine alipaswa kupewa na
mpenzi wake zaidi ya kupelekwa kwenye kisiwa hicho cha karafuu?
Nguo nyeupe likawa chaguo lao na picha zao zilizopigwa nyumba ya
mazingira ya kuvutia ya Zanzibar, zimeng’aa haswaa. Chini ni baadhi ya
picha hizo.
Kilio ACT ikipigania haki ya uchaguzi
-
CHAMA cha ACT Wazalendo kimesema safari ya kuitafuta haki ya uchaguzi
inaendelea. Lakini papohapo, kingependa kuona Mahkama
0 MAONI YAKO:
Post a Comment