
Tamasha Tigo Fiesta 2016 linaloendelea kutembea katika miji mbalimbali nchini, Linazidi kushika kasi katika maeneo linapokwenda. Kukiwa na matukio mbalimbali ya ya kijamii, lakini wasanii wakali nchini wanazidi kukonga nyoyo za mashabiki wao kwa kuwapa burudani kubwa za kufa mtu ambapo zinawafanya mashabiki wakonge nafsi zao. Tamasha hilo liliendelea tena usiku wa kuamkia leo katika mji wa Shinyanga uwanja wa nje wa Kambarage
Show kabambe ilidondoshwa kutoka kwa wasanii kama Fid Q, Darassa, MR. Blue, Dayna Nyange, Bill Nass, Madee, Linnah, Bonge la Nyau, Nikki wa pili, na wasanii wengine kibao

Dayna Nyange akikinukisha Shinyanga usiku wa kuamkia leo

MR. Skati Tamaa aka Darassa


Ngosha akisema na kina Ngosha Shinyanga

Mwana dada anayefanya poa sana katika Hip Hop anaitwa chemical

Mzee wa Ligi ndogo akikomelea jukwaani

Kipenzi cha madada, kipenzi cha wagumu hajawahi kuharibu jukwaani, Anaitwa MR.Blue Bayser akikamua kisawasawa hasa pale aliposema nao kwa mboga saba

Kama wewe unafuga nyau ila huwezi kumfguga huyu, anaitwa Bonge la Nyau

Mmoja ya wasanii wanaokuja kwa kasi sana katika game, ainaitwa moni centrozone

Ndege mnana naye alipata nafasi ya kufanya yake

katika kuvumbua vipaji, Fiesta hawajahi kuharibu, huyu anaitwa eduboy, siku zote huwa anajituma sana kuhakikihsa nasogea anapotaka.

Ubunifu wa hali ya juu uliofanywa na mdau wa Fiesta Shinyanga uliwakosha watu wengi sana hasa waandaaji wa Fiesta. Jamaa alichonga neno Imoooo! ambalo ndiyo kauli mbiu ya Fiesta 2016.

Moja ya maprisenter wanaofanya poa sana nchini toka Clouds TV anaitwa nicksongeorgekali

Kwenye mashine sasa, heeee!!!! mkali wa kali toka Clouds Media anaitwa DJ D Ommy, aliwafanya wakazi wa Shinyanga washinde kuondoka uwanjani
0 MAONI YAKO:
Post a Comment