
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya
Nikki wa Pili akiwafungua wakazi wa Tabora kwa kuwaonyesha fursa
wanazopaswa kuzitumia ili waweze kusukuma mbele maendeleo ya mkoa huo.

Msanii wa Muziki wa Kughani
Mashairi, Mrisho Mpoto akiwa amenyanyua mikono juu wakati akiwapa mbinu
za mafanikio wakazi wa Tabora.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh.
Aggrey Mwanri (wa nne kutoka kushoto), akiwa kwenye picha ya pamoja na
baadhi ya viongozi na wanasemina hiyo.

Mkurugenzi wa Vipindi na
Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba (katikati), akiongea jambo
mbele ya Mkuu wa Mkoa huo wakati akitoa somo la Fursa.

Mkuu wa Chuo cha Mlimani Professional Hassani Ngoma, akitoa soma la Fursa Ukumbini hapo.

Afisa Masoko wa kanda ya kati wa
NMB, Josephine Kulwa akiwapatia fursa wakazi wa Tabora namna wanavyoweza
kufaidika na fursa mbalimbali kwa kujiunga na baadhi ya huduma
zitolewazo na benki hiyo.

Mrisho mpoto akiwa ameketi na baadhi ya watu waliyohudhulia semina hiyo.

Baadhi ya wakazi wa Tabora waliohudhulia kwenye somo la Fursa wakinyoosha mikono kuashiria kuelewa kila wanachofundishwa.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Aggerey Mwanri, akiagana na Ruge baada ya kumalidhika kwa Fursa.

Mashindano ya kusaka vipaji yakiendelea.
MKUU wa Mkoa wa Tabora MH. Aggrey D.J Mwanri mapema leo alijikuta
akitoa ya moyoni kwa kuisifia kamati na uongozi mzima uliyoandaa tamasha
la Fiesta 2016 kwa kuwapelekea Darasa la Fursa.Akizungumza ndani ya Ukumbi wa chuo cha Uwaziri mjini Tabora wakati wa semina hiyo Mkuu wa Mkoa huo Mh. Aggery Mwanri alisema kuwa, amefurahishwa sana na uongozi mzima wa Fiesta kwa kuwawezesha wakazi wa mji huo kuwaonyesha namna ya kupambana kimaisha kwa kutumia rasilimali zilizopo mkoa hapo.
“Napenda kutumia muda huu kutoa pongezi zangu za dhati kwa waandaaji wa Tamasha la Fiesta hasa kupitia darasa hili la Fursa ambalo naamini wazi kabisa kila mmoja wetu aliyehudhulia hapa ataweza kujifunza na kuvuna mbinu mbadala za kujikwamua kimaisha na kuufanya Mkoa wetu wa Tabora kuongeza uajibikaji,”
Pia Mh. Mwanra aliwaomba wananchi wa mkoa huo kutumia fursa ya buruda zitakazo endelea usiku wa leo katika Uwanja wa Ali Hassani Mwinyi kwa kusitarehe na kuangalia vitu vya msingi vye kuwaongezea kipato zaidi.
Semini hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba ilionekana kuchangamka vilivyo na kuwafanya baadhi ya wahudhuliaji wakiwemo wanafunzi wa Chuo hicho kuomba darasa hilo liwe linawafikia mara kwa mara mjini hapo.






0 MAONI YAKO:
Post a Comment