Soko kuu la Morogoro kabla halijabomolewa
Kufuatia zoezi la ubomoaji ili kupisha ujenzi wa Soko jipya la mkoa wa Morogoro, kumetoa fursa kwa baadhi ya wakazi wa Morogoro kuitumia nafasi hiyo kujiingizia kipato kisicho rasmi. Mpiga picha wetu wa blog ya ubalozini, alitembelea katika maeneo hayo na kukuta vijana wakiwa katika harakati za kubomoa majengo hayo na kujipatia biashara isiyo rasmi. Baadhi ya vijana hao walionekana wakibomoa kuta za majengo hayo na kukusanya vitu kama Tofari, Nondo, Malumalu, mbao na kuviuza kwa wananchi wengine kwa ajili ya matumizi mengine. Tulijaribu kuwahoji kama wameajiliwa kwa kazi hiyo, walisema hawakuajiliwa kwa kazi hiyo, ispokuwa kutokana na ugumu wa maisha wameamua kujitolea kubomoa soko hilo na kuuza kile wanachoona kinahitajika kuuza.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment