October 13, 2016


Wiki hii nchi ya Burundi inazimiliki headlines za kutangaza kuwa bunge la nchi hiyo limepiga kura ya kujiondoa uanachama wake kwenye mahakama ya makosa ya jinai duniani ICC, Ripoti mpya kutoka mahakama hiyo zimesema kuwa Burundi imefanya haraka mno uamuzi huo, wakati tayari ina kesi ya kutumia majeshi yake kama chombo cha ukandamizaji.

Ikumbukwe kuwa baraza la Seneti limepiga kura ya serikali ya Burundi kujiondoa kuwa mwanachama wa ICC na tayari taarifa imemfikia Rais Pierre Nkurunziza kwaajili ya kutia saini.

Hii itakua ni kwa mara ya kwanza kwa mahakama hiyo kukutana na uamuzi wa nchi kujiondoa ingawa ripoti zinasema uamuzi huo hauizuii Burundi kutofunguliwa mashitaka mbele ya mahakama ya kimataifa.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa ICC Bensouda, anasema sheria za Roma zinaeleza kwamba uamuzi wa kujiondoa ICC unachukua mwaka mmoja baada ya tarehe ambayo uamuzi huo utakua umewasilishwa kwa vyombo husika, uamuzi wa kujiondoa hautakua na mabadiliko ya kesi ambazo tayari zinaendelea kushughulikia na taasisi hiyo ya kimataifa hata kama uamuzi huo utabatilishwa.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE