Tukio hilo la aina yake limetokea katika kata ya Muembesongo Mkoani Morogoro na kukusanya watu na kila mmoja alikuwa na maneno yake .Kwa mujibu wa wenyeji wanaomfahamu walisema, hii siyo mara yake ya kwanza kufanya tukio hilo katika mti ule mkubwa maarufu mkoani Morogoro. Wapo waliosema kwamba ni michezo yake mwenyewe huku wengine wakihusisha na imani za Kishirikina kwa kusema kwamba Juma Vigogo ana majini, kwa hiyo ule mti siyo mzuri kwani una mambo ya kishirikina. Mashuhuda ao waliongeza kusema kwamba Bwana Juma aliwahi kusema eti ipo siku atahakikisha ule mti anauangusha na kubakia kigogog tu kwa siyo mzuri hata kidogo hukuakisema kwamba eti kuna vitu vimechimbiwa katika eneo lile ambao siyo vizuri. Baada ya watu wa usalama kufika na kutaka kumshusha alikuwa akitembea juu ya mti akiama matawi na kuwafanya watu wakitengo cha zima moto,Tanesco na Polisi kushindwa kumshusha nakuwa na wakati mgumu juu yake.
Mpaka tunaondoka katika eneo la tukio majira ya 20:30 , zoezi la kumshusha halijafanikiwa
Gari ya TANESCO na vyombo vya usalama wakiangaika kumshusha bwana Juma Vigogo bila mafanikio baada ya kuwa akiwachezesha kwa kuhama matawi ili kuwakwepa
0 MAONI YAKO:
Post a Comment