October 23, 2016

Mbunge wa Mikumi mabaye pia ni msanii wa BongoFleva Joseph Haule Prof. Jay, ametoa msaada wa kiti mgonjwa aliyekaa ndani kwa miaka miwili. Katika ukurasa wake wa Facebook Prof. Jay ameandika

"Kupitia Taasisi yetu ya PROFESSOR JAY FOUNDATION tumefanikiwa kukabidhi WHEELCHAIR Kwa familia ya kijana ALLY MKINGI (23) ya kijiji cha KIFINGA kata ya RUAHA ambaye June mwaka 2014 aligongwa na gari la Polisi lililokuwa linaikwepa pikipiki iliyoingia ghafla barabarani, likaacha njia na kupinduka mara kadhaa na kumkuta kijana huyu aliyekuwa kando kabisa ya barabara akitembea kwa miguu.
Ally ameumia sana na kupooza kuanzia kifuani mpaka chini na bahati mbaya sana kukosa uwezo na msaada Zaidi alikuwa amelala ndani tu kwa zaidi ya miaka 2 na mwili wake ukaanza kuharibika vibaya kwa vidonda vikubwa, Pamoja na jitihada zetu kubwa za kumtibia lakini ripoti ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Muhimbili (MOI)wametuambia ALLY hataweza kurudi kwenye hali yake ya kawaida kwani muda umepita sana hivyo tuendelee kumtibia vidonda hivyo lakini pia wakatuambia vidonda hivyo vimesababishwa na kulala sana ndani na kujisaidia hapohapo kwa kutumia mipira hivyo kutengeneza unyevunyevu na wakatuambia ni vema tumnunulie wheelchair ili aweze kufanya mazoezi na pia kupata hewa ya nje mara kwa mara huku tukiendelea kumtibia na ndicho tunachokitekeleza..
Kijana Ally mwenye Mke na Mtoto mmoja amefurahi sana na sasa angalau anaweza kuonana na marafiki zake wa zamani ambao wengi hajaonana nao kwa muda mrefu lakini pia inampunguzia sana upweke aliokuwa nao wa kukaa ndani Peke yake bila kuwa na uhakika wa kesho yake. ..
Mungu ni mwema sana na tunamtumaini yeye tu ili aweze kurudisha furaha na faraja kwa kijana huyu anayeteseka sana na familia yake".

Pichani Ally na Mama yake mzazi na kaka yake mkubwa Abdalla ambaye ndie anamuhudumia kwa kila kitu wakiwa na Mbunge wa MIKUMI nje ya nyumba yao!!

Related Posts:

  • Msilipize kisasa: Malim Seif Katibu Mkuu wa CUF taifa Maalim Seif amewaasa wanachama wa cuf jimbo la Dimani kutolipiza kisasi kwa kitendo cha kuchomewa moto ofisi yao usiku wa kuamkia juzi. Maalim Seif ambaye ni makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar… Read More
  • CCM wamuonya Nape kauli zake kwa Lowassa   Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) MKoani Arusha, Robson Meitinyiki, amemtaka K… Read More
  • Aliyebaka mtawa akamatwa   Polisi nchini India wamemtia mbaroni mwanamume mmoja kuhusiana na ubakaji wa mtawa mmoja wa Kanisa Katoliki katika makaazi ya watawa Magharibi mwa Bengal. Viongozi wa Kikristo nchini India wamekosoa Serikali kwa k… Read More
  • Magazeti ya leo hii March 26 haya hapa Leo Alhamisi Tarehe 26 March 2015. Tunakupatia fursa ya kutembelea kurasa za magazeti ya leo hii kama tulivyoyapata … Read More
  • CUF waitaka tume ya Taifa kukili kushindikana kwa kura ya maoni Naibu mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama hicho ABDUAL KAMBAYA akizngumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam kuhusu mchakato mzima wa uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika mfumo wa kielecron… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE