Katika
kutekeleza hilo wafanyakazi wa NMB nchi nzima wakishirikiana na Kitengo
cha Miradi ya Kijamii cha benki hiyo watakuwa wakishirikiana kukusanya
pesa kwa ajili ya kutoa msaada.
Jambo
hilo litahusisha wafanyakazi kuchangishana pesa wao wenyewe na baada ya
kukamilisha mchakato huo, Kitengo cha Miradi ya Kijamii kitakuwa
kikiwaongezea pesa sawa na kiwango ambacho walichangishana.
Pia
tayari baadhi ya matawi ya NMB nchini yameshaanza kutekeleza mpango huo
ambao uewekwa na benki ya kusaidia sehemu ya jamii ambayo inaonekana
kuwa na uhitaji.
Baadhi
ya matawi yaliyofanya hivyo ni Tawi la NMB Sumbawanga ambalo kwa
kushirikiana na Kitengo cha Miradi ya Kijamii walipata 600,000 na
kununua mifuko 80 ya saruji na kuwapatia wahanga wa mvua iliyonyesha
mjini humo mwezi uliopita kwa ajili ya kufanya matngenezo ya nyumba zao
kwa sehemu zilizoharibika.
Meneja tawi la Sumbawanga akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Sumbawanga, Dk. Halfan Haule msaada wa mifuko 80 ya saruji.
Wahanga wa Sumbawanga wakiwa wamepokea mifuko ya saruji kutoka bank ya NMB ikiwa ni maadfhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja
Wafanyakazi
wa NMB kutoka Idara ya Wateja Binafsi waliwatembelea watoto wa kituo
cha Salvation Army kilichopo Kurasini, Dar Es salaam kama sehemu ya
kutimiza uwajibikaji wao kwa jamii iliyowazunguka na kuwakabidhi baadhi
ya mahitaji maalumu kwa ajili yao.
Wafanyakazi
wa NMB Tawi la Kilosa wakiwa na mtoto Sheila (aliyebebwa na meneja wa
Tawi Dismas Prosper) ambaye wamemsaidia Milioni 1.4 kwa ajili ya
kufanyiwa upasuaji wa mguu katika Hospitali ya CCBRT na kupewa mguu wa
bandia ambao utamwezesha kutembea na kucheza na wanafunzi wenzake.
Mfanyakazi wa NMB, Victor Rugeiyamu akikabidhi magodoro pamoja na mahitaji mengine ya wanafunzi wa Shule ya Viziwi Buguruni.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment