Mwanamuziki Michael Ray Stevenson ‘Tyga’, amefunguka kuwa amewahi
kuonywa kutoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Mwanamitindo Kylie
Jenner lakini cha ajabu hakuambiwa sababu za kuwa mbali na mwanamke huyo
hivyo akapotezea. Akizungumza na Jarida la Complex, Tyga alisema yeye alikuwa na
mapenzi ya dhati na mwanamke huyo lakini kila alipokutana na marafiki
zake walimtahadharisha kuwa mbali naye.
“Marafiki zangu wengi walikuwa wakinitahadharisha kuwa mbali na Kylie
bila kunipa sababu, nilishindwa kuwasikiliza kwani moyoni nilimpenda
sana,” alisema Tyga.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment