October 25, 2016


  
Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kupitia mwamvuli wao wa umoja wao wa UKAWA vimefungua kesi katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakiiomba mahakama kufuta uchaguzi uliomchagua Meya na naibu Meya wa manispa ya Kinondoni na kutaka urudiwe kwa kufuata kanuni na taratibu za kiuchaguzi zilizopo.

Akizungumza katika viwanja vya mahakama hiyo mwanasheria wa CHADEMA Mh John Malya amesema katika kesi hiyo wamewashtaki watu wanne akiwemo Meya wa manispa hiyo Benjamin Sitta na msimamizi wa uchaguzi.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Kinondoni Mh Mustapaha Muro na ambaye ni moja ya walalamikji katika kesi hiyo akiwa kama ni mgombea wa nafasi ya umeya amesema wamekimbilia mahakamani ili kupata haki yao.

Henry Kileo ni katibu wa chama hicho mkoa wa Kinondoni ambaye anawataka wananchi  kuwa watulivu wakati suala hilo lipo mahakamani na waamini kuwa haki itatendeka tuu.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE