
Universal Music Group ni label kubwa duniani ambayo huingiza mapato ya zaidi ya dola bilioni moja kila mwaka pia inamiliki label zingine kubwa au hufanya kazi na label zingine (ikiwemo Def Jam Records). Label maarufu za wasanii ambazo kazi za wasanii wake husambazwa na UMG ni pamoja na Aftermath Records ya Dr Dre, Shady Records ya Eminem, Kon Live Distribution ya Akon, Will.i.am Music Group, na zingine nyingine.
Diamond alikuwa na msimamo wa kutosainishwa na label yoyote labda kama mkataba ukiwa ni wa usambazaji pekee wa nyimbo za wasanii wa label yake ya WCB, ambao UMG umempa pia Roc Nation ni miongoni mwa label kubwa duniani zilizowahi kumtaka imsainishe lakini hakukubali kusainiwa nayo.
“Wakati nipo BET, Roc Nation walinifuata wakitaka wanisain, acha Roc Nation kuna baadhi ya record label nyingi sana kubwa, nyingi sana, tena hawanifuati hivi hivi, wananifuata na ofa,” Diamond alisema.
“Lakini kila kitu ni target, mimi siku yoyote ukisikia nimefanya kazi na label kubwa duniani, sio kuwa under record label, ila pointi yangu itakuwa kwamba kuona namna gani wanaweza kukuza muziki wangu kidunia zaidi, nitafanya kila kitu mwenyewe. Kupata collabo na msanii yeyote mimi naweza kupata sababu Kimarekani collabo sio story, hela yako, ni biashara, mtu hawezi akakupa bure mfanye nyimbo ili upate hela, ufanye show yeye anafaidika na nini?” aliongeza Diamond.
“Nataka mtu akinisaini, nataka muziki wangu uuzike kama wanavyouza wakina Kanye West, Jay Z. Sitoingia eti Diamond kaingia na record label fulani, WCB itaingia na kampuni fulani na ikiingia ni katika makubaliano ya kuuza muziki katika digital kuona ni namna gani muziki wangu utauza sehemu fulani kwa bei nzuri,”Diamond alimalizia kwa kusema kuwa kwenye album yake ijayo kuna nyimbo atakazowashirikisha Rick Ross na Rihanna.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment